• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Wananchi wa Hydom Waipongeza Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa Kusikiliza na Kutatua Kero Mbalimbali za Jamii Katika Mkutano wa Hydom Tarehe 03.03.2021

Kurushwa hewani: March 4th, 2021

Aliyesimama ni Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga Akiwa Katika Mkutano wa 

Kusikiliza na Kutatua  Kero za Wananchi Katika Mamlaka ya Upangaji ya Hydom tarehe 03.03.2021

Aliyesimama na Kushika "Mic" ni Mh. Mbunge Flatei wa Jimbo la Mbulu,  Akisalimia Wananchi  na Kutoa Ufafanuzi Juu ya Mustakabali wa Maendeleo ya Jamii Katika Jimbo la Mbulu na Hydom Kwa Ujumla wake.

Mh.Diwani Nasali Sule wa Kata ya Hydom Akitoa Ufafanuzi wa Maswala Mbalimbali Yaliyoulizwa Katika Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom

Aliyeshika "Mic" ni Mh.Mwenyekiti Elihuruma Manase wa Kijiji cha Hydom Akitoa Ufafanuzi wa Maswala Mbalimbali Yaliyoulizwa 

Katika Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom


Aliyeshika "Mic" ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndugu Horace Kolimba Akiwatambulisha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri

 ya Wilaya ya Mbulu Katika  Mkutano huo, Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom.

Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu Sule Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.

Aliyesimama Kushoto ni Mratibu wa Mfuko wa BIMA ya Afya ya Jamii  Ndugu Mtweve Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.

Aliyesimama Kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.

Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Ndugu M. Faray Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.




Wakwanza Kushoto ni Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga Akitoa Maagizo Katika Mkutano wa 

Kusikiliza na Kutatua  Kero za Wananchi Katika Mkutano Huo.

Aliyesimama Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Chitopela Akitoa  ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.

Aliyesimama Kulia ni Mwanasheria wa Wilaya Ndugu Mwambage Akitoa  ufafanuzi wa Sheria.

Aliyesimama Mbele ni Mratibu wa Mpango wa Kusimamia Kaya Maskini wa Wilaya "TASAF"  Ndugu Nguvava Akitoa  ufafanuzi Katika Mada Iliyohusu TASAF.

Aliyesimama Mbele ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu F. Kagenda Akitoa  ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.

Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Idara ya MIfugo Ndugu Nduligu Akitoa  ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.

Aliyeshika "Mic" ni Mkuu wa Idara ya Afya na Usafi wa Mazingira Ndugu Kilimba Akitoa  ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.

Aliyeshika "Mic" ni Afisa Elimu Kata wa Kata ya Hydom Mkuu Ndugu Helen Massay Akitoa  ufafanuzi Katika Mada ya Sekta ya Elimu Hydom.


Aliyeshika "Mic" ni Afisa Tarafa wa Tarafa ya Hydom Ndugu Benny Mwandelele Akitoa  ufafanuzi wa Suala la Tozo za Mazingira.



Hizo Hapo Chini ni Baadhi ya Picha za Wananchi wa Hydom Waliotoa Kero Mbalimbali Zilizosikilizwa na Kujibiwa Hapo Hapo.










~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~






Hayo yamejiri leo katika mkutano mkuu wa wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji (W)  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga, ambao uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kata ya Hydom kuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Kimsingi Mkurungezi huyu aliambatana na wataalamu wake wakuu wa Idara na vitengo vyote ili kutatua kero za wananchi wa Hydom pamoja na kutoa miongozo mbalimbali ya kiserikali ikiwemo sheria, afya, ardhi, mifugo, maendeleo ya jamii na kilimo.

Hata hivyo kikao hiki kimekuwa cha manufaa sana baada ya kila mwanachi aliyetaka kuuliza maswali aliuliza kisha ofisi ya mkurugenzi mtendaji ilitoa ufafanuzi wa kitaalamu hapo hapo wakati mengine yalipokelewa na kuendelea kuyafanyia kazi kwani yalihitaji ngazi zingine za maamuzi kama vile RUWASA, TARURA; muda na nyaraka zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Hudson Kamoga alitamka kwamba ni jukumu la kila mwananchi kila mwisho wa mwezi kufanya usafi katika eneo lake la biashara na nyumbani katika makazi yake, kila ofisi ya biashara kuhakikisha inakuwa na chombo cha kuwekea taka (dust bin) ili kurahisisha uzoaji wa taka hizo katika maeneo yote ya biashara na makazi. Serikali ya Kijiji cha Hydom iorodheshe majina ya wananchi wote waliohudumiwa na shirika la "FOCCP" lililokuwa linapima viwanja hapa kisha yaletwe ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ili taratibu za ufuatiliaji ufanyike baada ya wao hadi sasa kutojibu barua aliyowaandikia Shirika hili mwaka jana 2020.

Katika kujali wananchi na kukuza biashara Mkurugenzi Kamoga amesema, atahitaji kuwa na kikao na wafanya biashara wa Hydom kwani ni kitovu cha biashara katika Wilaya ya Mbulu kwa kuanzia na wamiliki wanaohusika na biashara za gesti ili kujua changamoto zao na kuweza kuzitatua kwani huu ndiyo utekelezaji wa Ilani ya Chama na Mapinduzi inayosimamiwa na kiongozi anayewajali wananchi na maendeleo yao Mh. Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. J. P. Magufuli.

Mgeni rasmi huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Ndugu Hudson Kamoga aliongeza kwa kutamka kuwa mwananchi hana mipaka katika kutoa taarifa zake ili aweze kutatuliwa kero, hivyo akipiga simu ngazi ya kitongoji hajaridhika au kutopata majibu afuatilie ngazi ya Kijiji kisha kata hadi Tarafani akishindwa maeneo yote hayo basi apige simu ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Katika kuhakikisha watumishi wa umma wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria; watumishi wote ni muhimu kuwa na lugha nzuri kwa wananchi lakini panapotokea lolote Afisa Mtendaji wa kata awawajibishe watumishi walio chini yake kwa mujibu wa sheria, tuwahudumie wananchi kwani sisi tuko kwa ajili yao na tunalipwa kwa kodi zinazotokana na kodi zao.

Ili kuwa na uwezo wa kufanya maendeleo mbalimbali ya kata na vijiji ni muhimu kuwa na takwimu sahihi ambapo imefahamika kwamba tayari Mamlaka ya upangaji ya Hydom wamejipanga kimkakati kupata idadi ya kaya sahihi na zoezi linaendelea ili isaidie katika kupanga na kufanya maamuzi mbalimbali ya maendeleo.
.
Kwa hali hii ili kudumisha utawala bora ni vizuri kila fedha zinapopatikana ni muhimu kuwapa taarifa wadau wakuu wa fedha hizi ambao ni wananchi wa kijiji au kata husika kupitia mbao za matangazo na mikutano mikuu ya vijiji kwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu ili kuwapa mrejesho wananchi na kujua fedha zimetumikaje, hii itaongeza imani ya wananchi katika serikali yao kuhusiana na uchangiaji chanya na endelevu wa miradi inayofuata.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iko karibu sana na makundi maalumu ya Wanawake, Vijana na walemavu kwa kuwapa mikopo; aidha, kupitia fedha za marejesho tumetoa kiasi cha shilingi 121,277,893/=  kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni vyanzo vya mapato ya ndani kwa 100% kwa lengo lililopangwa kwa vikundi 46, na mwaka huu wa fedha 2020/2021 unaoendelea hadi sasa tumetoa fedha kiasi cha shilingi 59,316,927/= kwa vingundi 15, na zoezi hili ni endelevu tunaendelea kutoa mikopo hiyo chamsingi ni kuandaa mihutasari ya vikundi na maandiko ya miradi husika kwa kupitia ngazi zote zinazohusika za mitaa kisha kufika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu pale Dongobesh ili kuweza kukamilisha zoezi la kupatiwa mikopo hiyo. Kuhusiana na michango mbalimbali Mgeni rasmi huo Ndugu Kamoga alimwagiza Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kukagua taarifa za michango ya wananchi na matumizi yake kuanzia wiki ijayokatika kijiji cha Hydom .

Katika kuupandisha hadhi Mamlaka ya Upangaji ya Mji wa Hydom na kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Hydom bado vigezo havijafikiwa hivyo wananchi waendelee kuongeza juhudi za kimaendeleo kwa kuongeza kituo cha afya cha serikali hivyo muone mkakati wa kuleta mihtasari ya kituo cha afya cha serikali kwa kuainisha wapi eneo limepatikana lisilo na mgogoro  na la ukubwa kiasi gani kisha tutashirikiana kwa pamoja kuona namna ya kupata fedha ili kituo kianze kujengwa mwaka huu 2021. Katika kufikia vigezo hivi ni pamoja na wananchi kupima na kulipia hati za viwanja vyenu ambapo ofisi mbalimbali na matumizi bora ya ardhi hupangwa, hadi sasa ujenzi wa Ofisi ya Mahakama ya Mwanzo unaanza ni mojawapo ya kushajiisha maandalizi ya mji huu.

Uongozi wa kata ya Hydom kupitia Mh. Diwani Nasaeli Safari Sule na viongozi wengine wa ngazi zote simamieni hili ili tuimarishe afya zetu kwa fedha kidogo kwa kituo cha afya cha serikali ukilinganisha  na Hospitali ya sasa ya Hydom inayotoa huduma nzuri lakini gharama ni kubwa na pia ni hospitali ya rufaa hivyo inatakiwa kupunguziwa mzigo wa wagonjwa.

Wananchi wote wa Hydom walimshukuru na kufurahi sana kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga kwa Kuwa na Moyo wa Huruma kwa kuwajali, kuwafuata na Kuwasikiliza kero zao na kuzitatatua. Wananchi hao wamekiri kuyapokea maagizo yote na kuyafanyia kazi ipasavyo ikiwemo suala la ujenzi wa kituo cha afya cha Hydom. Mh. Mbunge naye alishukuru sana kwa Mkurugenzi Kamoga na menejimenti yake kusikiliza kero hizi kwani kwa hali hii maendeleo yatawezekana.



















Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

    May 16, 2025
  • KAMATI LISHE YAKAA KIKAO CHA TATHIMINI YA HALI YA LISHE KWA ROBO YA TATU

    May 08, 2025
  • MADIWANI WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI KATIKA KATA ZAO

    April 29, 2025
  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.