Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Jackline David, amewaasa wanaume kuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye masuala ya lishe kwa ngazi ya familia na jamii ili kufuta tatizo la utapiamlo kwa watoto hasa wenye umri chini ya miaka mitano.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Idara ya Afya wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe katika kijiji cha Guye.
Hayo yamesemwa kwenye maadhimisho ya siku ya lishe yaliyofanyika siku mbili mfululizo ya tarehe 15-16/01/2025 katika vijiji vya uye na Qaloda ili kukamilisha robo ya pili ya mwaka.
“Watoto wengi wenye utapiamlo chanzo kikubwa ni baba kwa sababu wengi wao hawalei familia au ulevi uliokithiri na kumwachia mama shughuli zote za ulezi na uzalishaji.” Alisema Jackline David.
Pia alisema wanaume wengi wakiitwa kwenye vikao na mikusanyiko inayohusu lishe hawajitokezi kabisa au wanatokea kwa idadi ndogo kwasababu wanaona ni mambo ambayo hayawahusu kitu ambacho sio kweli kwani jukumu la lishe kwa familia linawahusu wazazi wote baba na mama.
Naye afisa lishe Lutengano Emmanuel, alisema kuwa familia zisiuze mazao yote wanayolima na kufuga kwa ajili ya kujipatia kipato bali wawe wanautamaduni wa kuacha na vya familia kwa ajili ya kula ili wajipatie afya bora.
Pia aliwahamasisha kulima na mazao ambayo huwa hawalimi lakini ni mazuri kwa lishe bora lakini pia ardhi yao inakubali.Aliyataja mazao hayo ni pamoja na ndizi,magimbi,choroko na njegere.
Naye mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Dr. Uyonyimoo Mchaki aliwaambia umuhimu wa kupanga uzazi na kutumia njia za uzazi wa mpango kama familia kwani kuna Imarisha afya ya mama na pia kuna mpa mtoto nafasi ya kunyonya kwa muda wa miaka miwili ambao unashauriwa na wataalamu.
Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Dr. Uyonyimoo Mchaki akitoa elimu kwa wanawake wa kijiji cha Guye.
Pia aliwasisitiza kina mama kuhudhuria kliniki mara wanapojigundua ni wajawazito na pia kuacha tabia za kujifungulia nyumbani kwa wakunga wa jadi kwani kunahatarisha afya ya mama na mtoto. Aliwashauri wanaume wawapeleke wenza wao kliniki ili wapokee ushauri wa wataalamu wakiwa pamoja hata mmoja akisahau mwingine atamkumbusha mwenzake.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.