Na. Nashon Biseko
One stop Center imeongoza Mafunzo ya Uelewa juu ya Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya Watoto katika jamii kwa Watumishi wa Serikali wa maeneo mbalimbali ya Wilaya na Mashirika Binafsi mapema hii leo tarehe 13/10/2025, Mafunzo haya yamelenga kuongeza uelewa juu ya kupambana na changamoto mbalimbali za Ukatili katika Jamii, Mafunzo haya yanatarajiwa kuisha tarehe 17/10/2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Mafunzo haya yamefunguliwa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Dr. Shadrack Makonda na Kuhudhuliwa na Maafisa Ustawi wa jamii, Watumishi wa Afya, Polisi, Maafisa Mashitaka (Wanasheria) na Wageni kutoka nje ya Nchi kwa lengo la kongeza uelewa katika jamii juu ya Ukatili wa kijinsia na Ukatili dhidi ya Watoto, Akisema ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa katika jamii zetu uwepo wa huduma mbalimbali kama huduma za afya, Ustawi wa jamii, Dawati la jinsia katika jengo moja imesaidia waathirika wa matatizo haya kupata huduma kwa urahisi.
Aidha, Daudi Donald ambaye ni mwendeshaji wa mafunzo haya Amesisitiza kuwa Mkoa wa Manyara ni Miongoni mwa Mikoa yenye changamoto za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto akiwataka Watumishi wote waliohudhulia kwenda kupambana na kuongeza uelewa katika jamii kwani tiba ya tatizo hili ni sisi wenyewe.
“Mkoa huu ni miongoni mwa mikoa yenye ukatili wa Kijinsia na tiba ya tatizo hili ni sisi wenyewe, Katika Ushiriki wa Mafunzo haya tayari umefunga Mkataba wa Kupambana na Ukatili katika Jamii” Alisema Donald
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.