Na, Ruth Kyelula, & Magreth Mbawala, Mbulu DC
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe.Prof. Kitila Mkumbo, jana Januari 2, 2025, amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wodi tatu, wodi ya watoto, wodi ya wanawake na wodi ya wanaume katika Hospitali ya Wilaya na pia aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mji wa Dongobesh.
Mhe.Waziri Kitila Mkumbo akizungumza na wananchi wakati wa kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa wodi tatu katika hospitali ya Wilaya ya Mbulu
“Mhe.Rais ameniagiza nije Dongobesh, nikague mradi huu, na nimpelekee taarifa kama mradi upo ama haupo, kwahiyo ndugu wananchi nimeridhishwa sana na utekelezaji wa ilani wa eneo hili, Lakini hongereni kwa kupata hospitali ya Wilaya.Maendeleo ndugu wananchi ndio haya, huduma kwa wananchi, kuweka miundombinu, kutengeneza mazingira ili wananchi wakae vizuri, wafanye shughuli za maendeleo” Alisema Mhe.Kitila Mkumbo.
Aliendelea kusema kuwa lengo la Serikali ni kuona kina mama wanajifungua salama, na akasema mwaka 2000 katika nchi hii katika kila wakina mama laki moja wanaojifungua, wakina mama Zaidi ya mia sita hamsini walikuwa wanafariki katika kila laki moja, wamepambana mpaka ilipofika 2022 wamepunguza toka 650 mpaka 104, lengo letu ni wakina mama wote wajifungue salama na ndio lengo la Mhe.Rais Samia.
Mhe.Kitila kwa upande wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami mji wa Dongobesh wenye gharama ya shilingi 474,975,000 aliwapongeza wana Dongobesh na kusema hiyo ni alama kubwa sana ya maendeleo katika eneo husika.
Mhe.Waziri Kitila Mkumbo akizungumza na wananchi wakati wa kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami mji wa Dongobesh
Kwa upande wa Mbunge wa Mbulu vijijini, Mhe.Flatei Massay alisema kuwa anamshukuru Mhe.Rais Samia kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo, katika kampeni zake za mwaka 2020, ujenzi wa lami km 4, katika mji wa Dongobesh, na kusema kuwa hatuna deni.
Naye Mhandisi wa Wakala wa Barabara za vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Mbulu, Nuru Hondo amesema kuwa hadi sasa mradi upo asilimia 70 ya utekelezaji, na mradi una gharama ya shilingi 474,975,000, na mpaka sasa mkandarasi yupo saiti anaendelea na kazi.Na alieleza mradi huo umeboresha sana mji wa Dongobesh.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.